UHIFADHI WA MAZINGIRA NA MALIASILI
News Training

UHIFADHI WA MAZINGIRA NA MALIASILI

May 14, 2026 By Rashid Ligaya

Mafunzo ya Uhifadhi maliasili na mazingira yatolewa kwa kamati ya maliasili na mazingira kijiji cha Lufulu kata ya Ching'anda ,Halmashauri ya Wilaya Mlimba.


Wataalam kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba kwa kushirikiana na Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro, Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na SUMAMA, wanaendelea kutekeleza mradi wa FOLUR kupitia zoezi la kurejesha uoto wa asili katika misitu ya vijiji sita vya Merera, Ching’anda, Lufulu, Udagaji, Mgugwe na Chisano. Mradi huu unalenga kuboresha mifumo ya chakula, matumizi bora ya ardhi na kurejesha misitu iliyoharibiwa. Katika vijiji vya Ching’anda na Lufulu, tayari kamati za maliasili zimeimarishwa kupitia mchakato shirikishi uliohusisha uchaguzi wa wajumbe 12 kwa kila kijiji, kwa kuzingatia usawa wa kijinsia na uwakilishi wa vitongoji, na majina yao kupitishwa katika mikutano mikuu ya vijiji kwa ushirikishwaji wa wananchi. Wajumbe hao pamoja na viongozi wa vijiji wanatarajiwa kupatiwa mafunzo maalum ya usimamizi endelevu wa rasilimali za misitu, maji na mazingira ili kuongeza ufanisi wa uhifadhi na maendeleo ya vijiji. Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo wa kulinda rasilimali kama misitu, mito na vyanzo vya maji kwa kuzingatia sheria na taratibu za mazingira. Kwa ujumla, mradi wa FOLUR chini ya uongozi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba, Ndg. Jamary Idrisa Abdul, umeleta mwamko mpya wa ushirikiano na uhifadhi wa mazingira, ukiwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika kulinda rasilimali zao kwa maendeleo endelevu ya jamii.
Back to News & Events
Details
Published Date:

May 14, 2026

Category:

News

Type:

Training