News
Mafunzo ya kilimo endelevu kwa Maafisa Ugani na Wakulima Halmashauri ya Wilaya Mlimba kupitia Mradi wa FOLUR
June 15, 2026
By Rashid Ligaya
Mafunzo ya kilimo endelevu kwa Maafisa Ugani na Wakulima Halmashauri ya Wilaya Mlimba kupitia Mradi wa FOLUR
Wakulima 150 katika ngazi ya kata,Maafisa Ugani 23,pamoja na Wakulima Viongozi 46 kutoka kata tano za kimkakati wamepatiwa mafunzo ya kilimo endelevu cha zao la mpunga chini ya mradi wa FOLUR katika Halmashauri ya Wilaya Mlimba.Mafunzo haya ya uandaaji wa kitalu mkeka na usawa wajinsia yanashirikisha wataalamu kutoka kongani za Zanzibar na Mlimba yakiongozwa na Mtalaamu wa Uzalishaji wa Mpunga kutoka Makao Makuu ya Mradi,Wizara ya Maliasili na Utalii, kwa lengo la kuongeza tija na kulinda ikolojia ya bonde la Kilombero