News
Training
MAFUNZO YA KALENDA YA MSIMU WA MAZAO KATIKA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI
June 17, 2026
By Rashid Ligaya
Katika kuhakikisha wakulima wa Halmashauri ya Wilaya Mlimba wanakabiliana na mabadiliko ya tabianchi wakulima na Maafisa Ugani wamepata mafunzo ya kalenda ya msimu wa Mazao kwaajili ya zao la Mpunga.Hatua hii ya Mradi wa FOLUR inalenga kumuondoa Mkulima kwenye Kilimo cha mazoea na kumuwezesha kupanga ratiba sahihi ya uzalishaji ili kuongeza tija.
Mafunzo ya vitendo ya uandaaji wa kalenda ya msimu kwaajili ya zao la mpunga yamekamilika kwa wakulima na Maafisa Ugani katika kata tano nufaika na mradi wa FOLUR(Chisano,Mngeta,Mchombe,Ching'anda na Mofu).
Maafisa Ugani na Wakulima wakishirikiana kwa vitendo kuchora na kuandaa kalenda ya Msimu wa Mpunga.