News
Article
KIKAO KAZI CHA KUTATHMINI UTEKELEZAI WA MRADI KWA MWAKA WA FEDHA ULIOPITA (2025/2026)
July 06, 2026
By Anangisye Mwateba
Kikao kazi cha kutathmini utekelezai wa mradi kwa Mwaka wa Fedha uliopita (2025/2026) na kujadili Mpango wa Mwaka mpya wa Fedha (2026/2027).
Watumishi wa Mradi wa Mifumo ya Chakula, Matumizi ya Ardhi na Urejesho wa Mandhari ya Misitu nchini Tanzania (FOLUR) wamekutana jijini Dar es Salaam kutathmini utekelezai wa mradi kwa Mwaka wa Fedha uliopita (2025/2026) na kujadili Mpango wa Mwaka mpya wa Fedha (2026/2027).
Akizungumza katika kikao hicho, Mratibu wa Mradi huo Bw. Wanjala Mgaywa, alieleza kuwa kujadiliana kwa pamoja matokeo na changamoto walizokutana nazo kunawapa fursa watumishi kutoka kongani zote mbili za Zanzibar na Mlimba kuwa na uelewa wa pamoja.
“Hii inawawezesha kubuni mbinu mpya za kukabiliana na changamoto hizi."
Aidha, alibainisha kuwa utekelezaji wa shughuli hizo unazingatia usimamizi jumuishi wenye lengo la kuboresha, mifumo ya chakula, matumizi bora ya ardhi, usalama wa mazingira ya jamii na uhifadhi endelevu wa misitu," alisema Bw. Wanjala