Event
Other
WATUMISHI FOLUR WATEMBELEA MAONESHO YA 50 YA SABASABA
July 08, 2026
By Anangisye Mwateba
Watumishi wa Mradi wa Folur kwa Kongani za Zanzibar na Mlimba wametembelea maonesho ya 50 ya sabasaba kwa lengo la kujifunza fulrsa mbalimbali zinazopatikana katika taasisi zilizochini ya wizara ya Maliasili na Utalii.
Mratibu wa Mradi wa Mifumo ya Chakula, Matumizi ya Ardhi na Urejeshaji wa Mandhari ya Misitu (FOLUR) Bw,Wanjala Mugahya akiwa ameambatana na watumishi wa mradi kutoka Kongani za Zanzibar na Halmashauri ya Mlimba wametembelea banda la Wizara ya Maliasili na Utalii katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
Katika ziara hiyo, wamepongeza ubunifu na ubora wa bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na Taasisi mbalimbali zilizo chini ya wizara kutokana na mazao ya misitu, zikionyesha mchango wa sekta ya misitu katika kuongeza thamani ya rasilimali, kukuza uchumi na matumizi endelevu ya misitu.
Pia walipata wasaa wa kutembelea eneo la wanyama na kujifunza fursa mbalimbali kwenye masuala ya utalii, uwekezaji kwenye mashamba ya wanyamapori.